Jose Mourinho to Man United – Done Deal
Hatimaye tetesi zinageuka kuwa kweli, Manchester United watamtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao, shirika la utangazaji la Uingereza BBC limeripoti.
Huku United wakiwa wameshindwa kufuzu kucheza Champions League chini ya Louis van Gaal – viongozi wa Old Trafford wameamua kufanya mabadiliko.
Inaeleweka dili na kocha huyo mwenye miaka 53 lilifanyika kabla ya mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace.
United wanategemewa kumtangaza rasmi Mourinho mapema wiki ijayo baada ya kumtaarifu Van Gaal kuhusu mwisho wa ajira yake.
Van Gaal bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa miaka 3, lakini pamoja na kutumia £250m utawala wake umekuwa wa majuto kwa klabu na kuwaacha mashabiki wengi wakiwa hawaridhiki na utendaji wake, msimu wa kwanza alimaliza nafasi ya 4, na msimu huu watano.
No comments: