Home
Unlabelled
KAULI YA DEWJ BAADA YA SIMBA KUMALIZA MSIMU BILA TAJI
KAULI YA DEWJ BAADA YA SIMBA KUMALIZA MSIMU BILA TAJI
Msimu wa 2015/2016 wa Ligi Kuu sokaTanzania ndio ulikuwa msimu ambao Simbawamepewa majina ya utani mengi zaidi kutoka kwa wapinzania wao wa jadi klabu ya Dar es Salaam Young Africans, hii ilitokana na kukubali vipigo mara katika mechi za mzunguuko wa kwanza na wa pili.
Leo May 22 2016 Simba imemaliza mechi yake ya 30 ya Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa kucheza dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kukubali kipigo cha goli 2-1, mechi ya leo ilikuwa ni mechi ya 6 kwa Simbakufungwa katika mechi zake 30 ilizocheza msimu huu.
Baada ya kipigo hicho mashabiki na wapenzi wa timu hiyo walionesha kuumizwa na matokeo hayo, mmoja kati ya watu walioumia ni bilionea kijana Afrika Mohamed Dewjialiyeamua kutumia account yake ya twitterkuonesha hisia zake na matokeo ya timu hiyo “#Simba mnatunyima raha, tumechoka kutaniwa na kutukanwa mitaani”
Kama utakuwa na kumbukumbu nzuriMohamed Dewji aliwahi kuomba kuinua Simba, ombi ambalo liliifanya klabu hiyo kuwa kwenye headlines kwa muda mrefu, Dewji pia March 24 2015 alitajwa na jarida la Forbes kama bilionea wa 24 Afrika kati ya mabilionea 29, lakini yeye ndio alikuwa bilionea kijana kuliko wote akiwa na utajiri unaofikia trilion 2.43 za kibongo.
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2
U
KAULI YA DEWJ BAADA YA SIMBA KUMALIZA MSIMU BILA TAJI
Reviewed by Unknown
on
Sunday, May 22, 2016
Rating: 5
No comments: