SERIKALI: WANASIASA NDIYO WAMEIKWAMISHA BOMBADIER
Serikali imekiri dosari kuukumba mchakato wa ununuzi wa ndege ya tatu aina ya Bombadier iliyokuwa itue nchini mwezi Julai mwaka huu huku ikiwataka watanzania kuwa watulivu kwa kuwa ndege hiyo ipo na itakuja nchini mara baada ya kutatuliwa kwa mambo yaliyokwamisha mpango huyo.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa idara ya habari Zamaradi Kawawa amesema ununuzi wa ndege hiyo umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania.
"Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia. Hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili. Ndege ya tatu ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini serikali yao" Amesema Zamaradi Kawawa.
Amesema serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi na kuwataka watanzania kuwa wazalendo katika kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo
No comments: