UJUE UGONJWA WA KISUKARI
Kisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu.
Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukabili insulini.
Dalili za kisukari
• kukojoa kupitia kiasi cha kawaida
• kiu kikubwa
• kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu
• kuchoka haraka
• vidonda vinavyopoa polepole mno hasa kwenye miguu hadi kupotea viungo
• Kiu kikali cha mara kwa mara
• Njaa kali ya mara kwa mara
• Kupungua kwa uzito
• Uchovu
• Maambukizi ya mara kwa mara
• Kutapika kunako ambatana na maumivu ya tumbo
Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Watu walio wengi wana udhaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja mafuta mabaya mengi katika chakula na vyinywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kushika kisukari kuanzia baada ya miaka ya ujana

Ugonjwa wa kisukari ni mlolongo wa matatizo mwilini, ya muda mrefu na mfupi kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa insulin.
Insulin hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya kiungo cha kongosho. Miili yetu inahitaji insulin ili kuweza kutumia sukari tuliyonayo mwilini. Sukari inatokana na chakula ambacho tunakula kila siku na hutumika kwa kutupa nguvu mwilini. Kwa kawaida sukari ikizidi ya ziada inahifadhiwa katika ini kama mafuta.

Mafuta haya hubadilishwa kuwa sukari na kutumika wakati tukiwa na njaa kwa mda mrefu.
Endapo kuna matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulin, sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa kisukari upo na dalili kuanza kuonekana.
VIASHIRIA VYA UGONJWA WA KISUKARI (RISK FACTORS)
• Unene uliozidi na kiribatumbo
• Ulaji mbaya wa chakula
• Baadhi ya madawa
• Msongo wa mawazo
• Historia ya ugonjwa wa kisukari kwenye familia
• Tezi ya shingo (husababisha mwili kukua na kuongezeka haraka)
• Kutofanya mazoezi Umri zaidi ya miaka arobaini (kadri tunavyozeeka na kongosho letu linapungua uwezo wa kutoa insulin hivyo kusababisha kisukari)
• Magonjwa yanayoharibu kongosho Akina mama wanaojifungua watoto wenye kilo nyingi, na wenye umri Zaidi ya arobaini (Mara nyingi hawa akina mama huwa na ugonjwa wa kisukari ila hawagunduliki hadi mtoto anapozaliwa na kuonekana mkubwa)
• Akina mama wenye historia ya kisukari wakati wa ujauzito
TIBA YA UGONJWA WA KISUKARI
• Tiba bila dawa- ukigundulika unatakiwa kula chakula utakachoshauriwa na kufanya mazoezi ili ili kushusha sukari yako iwe ya kawaida.
• Tiba kwa vidonge-wengine hawawezi kutumia chakula tu kwa kushusha sukari hivyo wanapewa dawa za vidonge ili kushusha sukari yao pamoja na chakula.
• Tiba kwa kutumia sindano ya insulin
MADHARA YA UGONJWA WA KISUKARI
Endapo ugonjwa wa kisukari utapuuzwa au kutotibiwa inavyostahili madhara mengi yanaweza kujitokeza na yanatokana na kiwango cha sukari kuwa juu mwilini.
■Magonjwa ya moyo
■Kiharusi
■Kupungua nguvu za kiume
■Figo kushindwa kufanya kazi
■Upofu
Ni matumaini yangu wewe msomaji umenufaika na hili somo na pia utanufaisha familia na jamii iliyokuzunguka.
Kama hujapata huu ugonjwa ni muhimu kuepuka unene uliozidi kwa kula lishe nzuri na ya kiasi, epuka pombe, msongo wa mawazo, pombe na uvutaji wa sigara na la muhimu zaidi ni mazoezi ya viungo.
Tunashauriwa kupima kama tuna ugonjwa wa kisukari kila mwaka, hivyo basi nenda mapema ili kuepuka madhara.
Tunatoa mwongozo kuhusiana na Lishe sahihi itakayokuondolea madhara ya ugonjwa huu wa Kisukari na hata nguvu za kiume kukurejea vizuri kwa wanaume.

No comments: