Friday, February 28 2025

Header Ads


AJALI YA NDEGE YAUA WACHEZAJI BRAZIL

Bogota, COLOMBIA

ZAIDI ya watu 25 wakiwemo wachezaji wa klabu ya Chapecoense ya nchini Brazil wanasadikika kufariki dunia katika ajali ya ndege iliyobeba abiria 72. Chapecoense walikua wanategemewa kucheza mechi yao ya kwanza ya kombe la Sudamericana dhidi ya Atletico National katika dimba la Estadio Medellin Atanasio Girardot jumatano hii.

 Ndege hiyo ilipata ajali ikiwa inaelekea Santa Cruz De La Sierra mjini Bolivia. Mamlaka ziliripoti taarifa ya dharula majira ya wa saa 4 usiku ikiwa saa 12 asubuhi kwa saa za Afrika mashariki huku ikielezwa kuwa ilisababishwa na hitilafu ya umeme.

Ndege hiyo inaaminika kupata ajali katika manispaa ya Cerro Gordo, La Union na Meya wa mji huo alisema "Inaelekea wamefariki watu wengi, zima moto wametutaarifu kuWa hadi sasa wanafikia 25 hadi 27 ingawa Polisi wa Medellin imetaarifu vifo 75 na waliosalimika 6.

Shirikisho la soka barani Amerika Kusini CONMEBOL limesitisha shughuli zote mpaka kutakapotoka taarifa nyingine.

No comments:

Lazaro Masika. Powered by Blogger.