HILI NDIO JAMBO ALILO LIFANYA MKAPA NA KUPELEKEA MWALIMU
( NYERERE ) AMUITE NYUMBANI KWAKE ( MSASANI ) HARAKA SANA!
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. |
MKAPA NA KUITWA MSASANI.
“ MWAKA 1965 nilikubali ombi la uongozi wa Shirika la Utangazaji la Tanganyika ( TBC) kusoma taarifa ya habari kwa lugha ya kiingereza. Siku moja baada ya kusoma taarifa ya saa moja usiku, ilipigwa simu chumba cha habari, ikiniagiza niende mara moja Msasani ( nyumbani kwa Mwalimu ) kwani Rais alitaka kuniona.
Rais Mstaafu Mh. Mzee Benjamin William Mkapa. |
Moyo ulidunda lakini nilipo wasili Mwalimu alinituliza akaniambia anataka nikubali wadhifa wa kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya chama ( TANU ) ya Nationalist na Uhuru “
Maneno hayo ni ya Rais wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa, na yamo katika waraka wake wa Desemba 2011 alioliandikia gazeti la Uhuru wakati likisherehekea miaka 50 tangu lianzishwe.
Mbali ya kuongoza magazeti hayo, Mzee Mkapa alipata pia kuwa Waziri wa Habari na pia Waziri wa Mambo ya Nje. Ali iongoza Tanzania kama Rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Nyerere alimpigia kampeni ya nguvu mwaka 1995 ambapo alipata ushindi wa kishindo.
Inatoka kwenye gazeti la Raia Mwema, toleo Na. 346, Jumatano Aprili 9, 2 014.
No comments: