DoneDeal: Neymar asaini mkataba na PSG hadi 2022
Baada ya wiki mbili za habari zilizojawa na tetesi na fununu nyingi hatimaye usiku huu wa leo Alhamisi August 3, 2017 mshambuliaji wa Kibrazil Neymar Dos Santos amesaini rasmi kujiunga na PSG.
Taarifa kutoka klabu hiyo ya nchini Ufarsansa inasema PSG wana furaha kwa mshambuliaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitano katika klabu yao mkataba ambao utaisha 30 June 2022.
Neymar ambaye aliifungia Barcelona mabao 105 anataraji kuwa mhimili wa PSG na kuwa mchezaji wa kutumainiwa tofauti na alivyokuwa Barca akicheza chini ya mfalme Lionel Messi.
“Nina furaha kujiunga na PSG, toka nimekuja Ulaya kutokea Brazil klabu hii imekuwa moja kati ya vilabu vinavyofanya vizuri sana na hicho kimenifanya mimi kuja hapa,” alisema Neymar.
“Nipo barani Ulaya kwa miaka minne sasa na nimejifunza changamoto nyingi na hizo zitanisaidia kufanya kila niwezalo kuipa PSG makombe zaidi ili mashabiki wafurahi” alimalizia Neymar.
Naye mmiliki wa klabu ya PSG Nasser El Khaifi amemuelezea Neymar kama mchezaji bora sana na mwenye uwezo mkubwa huku akisema ni furaha kwa kwao kuwa naye na wanamkaribisha.
Usajili wa Neymar uligubikwa na mambo mengi sana kubwa ni kuhusu dau la £222m ambalo PSG wametoa kwa Barcelona, bado chama cha soka barani Ulaya kinaendelea na uchunguzi kuhusu kukiukwa kwa sheria za matumizi katika usajilu huu.
No comments: