Header Ads


Breaking News
recent

FAHAMU ATHARI ZA UGUMBA NA TIBA ZAKE


Ugumba ni tatizo ambalo limekuwa likiikumba jamii zetu mbalimbali kwa muda mrefu sana, na kwa kiasi kikubwa wanawake wamekuwa wakitupiwa lawama kuwa wao ndio sababu ya kukosa mtoto! Ukweli ni kwamba tatizo hili la ugumba linaweza kusababishwa na mwanaume au mwanamke! Miaka ya hapa karibuni taizo hili limekuwa likiongezeka zaidi sehemu mbalimbali duniani ikiwemo na hapa nchini.

Tafiti zinaonesha asilimia 12 mpaka 28 ya wenzi duniani wanakadiriwa kuwa na tatizo la ugumba, na asilimia 40 ikisababishwa na wanaume, 40 wanawake na 20 ikiwa ni mchanganyiko wa matatizo kwa mwanaume na mwanamke. Njia mbalimbali za kutibu tatizo hili zimebuniwa na kusaidia watu wengi.

UGUMBA NI NINI?

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Hali hii inaweza kutokea kutokana na mwanaume au mwanamke, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo.

UTASA NI NINI?

Utasa ni hali ya mwanamke kutoweza kabisa kushika ujauzito au mwanaume kutoweza kabisa kusababisha ujauzito kwa mwanamke.

KUNATOFAUTI GANI KATI YA UGUMBA NA TASA?

Mtu tasa hana uwezo wa kupata mimba au kumpa mtu mimba kabisa, wakati mgumba ana uwezo wa kuja kupata mimba iwapo tatizo likaondolewa.

NINI HUSABABISHA UGUMBA?

Kuna sababu mbalimbali ambazo huweza kupelekea ugumba kwa mwanaume au mwanamke, tutaenda kuona baadhi ya sababu ambazo hujitokeza mara kwa mara.

WANAUME

Tatizo la ugumba kwa wanaume mara nyingi hutokana na kiasi kidogo cha mbegu za kiume, mbegu za kiume zinazoshindwa kutembea, mbegu za kiume zenye umbo lisislo la kawaida na kuziba kwa mijira ya mbegu za kiume.

Tatizo kwenye mbegu za kiume linaweza kutokana na;

Kuvuta sigara
Dawa kama matumizi ya bangi kwa wingi,
Mionzi
Unywaji wa pombe
Kemikali kama DDT, risasi (lead)
Kuziba kwa mirija ya kupitisha manii na shahawa; mbegu za kiume zinashindwa kupita.
Wanawake

Ugumba kwa wanawake mara nyingi hutokana na sababu kuu mbili ambazo ni;

Kuziba kwa mijrija ya kupitisha mayai
Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi.
Mirija ya kupitisha mayai inaweza kuziba kutokana na;

Ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambao unatokana kuwa na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama kisonono na klamidia.
Utoaji mimba usio salama (unsafe abortions)
Upasuaji maeneo ya kiunoni
Ugonjwa wa endometriosis
Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi inaweza kutokana na;

Umri mkubwa wa mwanamke, hasa miaka 35 – 40 na kuendelea.
Uvutaji wa sigara
Saratani ya Ovari
Mionzi
Ugonjwa wa Polycystic ovarian disease
Sababu nyingine za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa;

Makovu katika mji wa uzazi kutokana na kutoa mimba.
Mabonge ya kizazi (fibroids)
Kuziba kwa shingo ya uzazi
Kulegea shingo ya uzazi
Kisukari
Matatizo ya tezi ya shingo
Kufanya mazoezi ya kupitiliza (excessive exercising)
Tabia Hatarishi

Tabia hizi huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata hali ya ugumba au utasa maishani mwake;

Kutoa mimba kiholela, hupelekea kuwa na makovu katika mji wa uzazi na kulegeza shingo ya uzazi.
Magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa, hupelekea mirija kujaa maji au kuziba kwa makovu baada ya maambukizi kuisha.
Kufanya kazi kwenye mazingira yenye joto kali sana, hii huathiri zaidi wanaume. Hupelekea utengenezwaji wa mbegu ambazo ni chache au hazina nguvu za kutosha kurutubisha yai la mwanamke.
Uvutaji sigara
Vipimo Vya Kujua Ugumba

Vipimo mbalimbali vinapatikana ili kuwezesha kujua tatizo la ugumba linatokana na nini. Licha ya uwezo wa vipimo hivi, sababu ya ugumba katika asilimia 10 au zaidi ya watu wenye tatizo hili inaweza isijulikane kabisa. Ni vizuri kwa wenzi wote wawili wenye tatizo hili kuonana na daktati kwa ajili ya ushauri na vipimo.

Kwa wanaume hufanyika;

Kipimo cha manii (seminalysis) kuona kama manii zipo za kawaida na kwa kiwango kinachoatakiwa. Manii huchukuliwa kwa kondomu maalum wakati wa kufanya mapenzi au kwa kupiga punyeto.
Homoni za kiume kwenye damu; kipimo hiki hupima homoni za testosterone na Follicle Stimulating Hormone(FSH) ambazo huusika katika utengenezaji wa mbegu za kiume.
Kwa wanawake kuna vipimo vingi ambavyo huweza kufanyika, vikiwemo;

Hysterosalpingography – hutazama mirija ya uzazi (falllopian tubes) kama imeziba au la. Pia huonesha kama tumbo la uzazi lina vivimbe.
Ultrasound – kipimo hiki huonesha kama kuna vivimbe kwenye tumbo la uzazi, pia kwenye ovari kama kuna magonjwa yanayoweza kusababisha ugumba kama polycystic ovarian syndrome.
Homoni za kike katika damu – kipimo hiki hupima homoni za oestrogen na Follicle stimulating hormone ambazo huuusika kwenye kuandaa yai la uzazi kutoka kwenye ovari na upandikizaji kwenye mji wa uzazi.
Endometrial biopsy – tishu za mji wa uzazi huchukuliwa kuchunguza kama yai la uzazi limetoka. Pia huweza kuonesha kama kuna saratani ya mji wa uzazi au vinyama kwenye mji wa uzazi.
Matibabu ya Ugumba

Sababu ya ugumba inapojulikana matibabu yanaweza kufanyika na hali hii ikaisha, ingawa wengine licha ya sababu kujulikana bado wanaweza kushindwa kupata watoto baada ya matibabu hayo. Hivyo, matibabu ya tatizo hili yanahitaji uvumilivu na uelewa kuwa wakati mwingine yanaweza yasiwe na mafanikio haraka au kabisa kama tunavyotarajia. Kuna njia mbalimbali za kutibu ugumba, hizi zote zikijumuisha kuondoa tatizo linalosababisha mimba ishindwe kutunga au kusaidia mimba itunge.

Kuna njia za upasuaji hasa pale ambapo kuna vivimbe kwenye tumbo au mirija kuziba, dawa kwa ajili ya kusaidia mayai ya uzazi yatoke na teknolojia za kusaidia kuzaa (assistive reproductive technologies). Pia ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya ni sehemu muhimu ya matibabu, ukijumuisha siku ambazo ni rahisi mwanamke kushika ujauzito.

Upasuaji.

Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushikamana huweza kutibiwa kwa njia za upasuaji. Matibabu haya husaidia kuongeza uwezekano wa wenzi kupata mtoto.

Dawa.

Matatizo ya ugumba yanayotokana na ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi huweza kutibiwa kwa dawa. Dawa hizi hutumika kuziwezesha ovari kutoa mayai ya uzazi ili yaywe tayari kurutubishwa. Mara nyingi huweza kusababisha kutoa mayai mengi katika mzunguko mmoja na kusababisha ujauzito wa watoto wengi (mapacha au zaidi) pale yanaporutubishwa.

Teknolojia za kusaidia kuzaa (assistive reproductive technologies).

Hizi ni njia za kitaalamu ambazo zinatumika kusaidia wenzi kupata ujauzito kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke. Njia hizi ni kama Artificial Insermination na In Vitro Fertilization.

Artificial Insermination. Njia hii hutumika pale ambapo mbegu za kiume zipo kwa kiasi kidogo. Mbegu za kiume hukusanywa na kuingizwa kwenye mji wa uzazi kwa njia za kitaalamu.
In Vitro Fertilization. Njia hii hutumika hasa pale mirija ya mwanamke imeziba kabisa. Mayai na mbegu za kiume hukusanywa kitaaalamu na kisha yai kuchavushwa. Baada ya hapo yai lililochavushwa hupandikizwa kwenye mji wa uzazi.
Kuongeza uwezekano wa kupata mtoto na mwenzi wako, inashauriwa;

Acha kuvuta sigara.
Punguza vinywaji vyenye caffeine.
Kufanya mapezi siku 1 kabla ya yai kutoka (ovulation).
Kuacha kusafisha ukeni kwa kemikali (douching).
Njia za Kuzuia Ugumba

Pata matibabu ya magonjwa ya kisukari, tezi ya shingo(thyroid) na magonjwa ya zinaa kama unayo.
Pata mlo kamili wenye virutubisho vya kutosha hasa mlo wenye mboga za majani na matunda kwa wingi.
Acha kuvuta sigara
Acha unywaji holela wa pombe
Tatizo hili huathiri wenzi wengi kisaikolojia kwa kuleta hasira, majuto, msongo wa mawazo na hata kusababisha mvurugano katika mahusiano yao. Katika nchi zetu za kiafrika, wanawake wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili. Ni vizuri wenzi washirikiane katika hili, kwa kupeana moyo na kufuatilia matibabu kwa pamoja. matibabu yanaposhindwa kabisa kuleta mafanikio, wenzi wanaweza kuasili mtoto/watoto kama watakuwa na utayari.
0717035770 au 0753692612

No comments:

Lazaro Masika. Powered by Blogger.