Header Ads


Breaking News
recent

Yaliyowahi kutokea kwenye El Clasico




Ni El clasico nyingine ambayo itafanyika siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Camp Nou kati ya FC Barcelona dhidi ya wapinzani wao wakubwa kwenye soka la nchini Hispania, Real Madrid.
Madrid wataingia na ari kubwa kwenye mchezo huu wakiwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 33 baada ya kucheza michezo 13 wakishinda mechi 10 na kutoka sare mechi 3.
Lakini kwa upande wa Barcelona sare waliyopata kwenye mchezo wa mwisho ligi kuu nchini humo dhidi ya timu ya Real Sociedad hawiwezi kuwakatisha tamaa kuelelea mchezo huo wa Jumamosi. Pointi tatu zitawasaidia kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao waliopo kileleni mwa msimamo
Barca wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 27 baada ya kushinda mechi 8 kwenda sare 2 na kufungwa 3.
Mbali na matokeo ya uwanjani mchezo huu umekuwa ukiacha kumbukumbu muhimu kila unapomalizika. Makala hii inakupa kwa ufupi baadhi ya kumbukumbu ambazo zimewahi kuwekwa kwenye El Clasico katika mtindo wa namba

NAMBA 2 (LIONEL MESSI, FERENCE PUSKAS)
Ni wachezaji wawili tu kwenye historia ya mchezo huu ambao wamewahi kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja zaidi ya mara moja. Ni Lionel Messi ambaye anaendelea kucheza hadi sasa pamoja na mchezaji wa zamani wa Barca Puskas.
Messi na Puskas wote wamewahi kufunga hat trick mara mbili kwenye El Clasico.

NAMBA 3 (INIESTA, RONALDINHO, CUNNIGHAM)
Wazungu wanaita Standing Ovation kile kitendo cha mashabiki kusimama ikiwa ni ishara ya kumpa heshima mchezaji wakati anatoka uwanjani. Ni ngumu kwa mchezaji wa Barca kupewa heshima hii kwenye uwanja wa Bernabeu, pia kwa mchezaji wa Mardid kwenye uwanja wa Camp Nou.
Lakini kuna wachezaji watatu ambao wamewahi kupewa heshima hii ambao ni Iniesta mwaka 2015 Barca ikishinda 4-0, Ronaldinho Gaucho mwaka 2005 Barca ikishinda 3-0 na Laurie Cunnigham mwaka 1980 Mardid ikishinda 2-0

NAMBA 14 (LIONEL MESSI)
Lionel Messi anashika nafasi ya kwanza kwenye chati ya ufungaji bora wa muda wote kwenye mchezo wa El Classco. Hadi sasa amefunga mabao 14 kwenye ligi kati ya Barca dhidi ya Mardid pia ana jumla ya mabao 21 kwenye mashindano yote kwenye mchezo ambao ulihusisha Mardid na Barcelona.
Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao 8 kwenye ligi mabao 16 kwenye mashindano yote. Nafasi ya pili inashikwa na mchezaji wa zamani wa Mardid Alfred De Stefano

NAMBA 33 (ANDRES INIESTA)
Kwa wachezaji ambao wanaendelea kucheza hadi sasa, Iniesta ndiye mchezaji aliyecheza michezo mingi ya El Clasico akiwa na jumla ya mechi 33. Akishika nafasi ya sita kwenye orodha ya muda wote ya wachezaji waliocheza El Clasico nyingi

NAMBA 93 (REAL MADRID)

Real Madrid inaongoza kushinda mechi za mashindano za pambano la El Clasico. Madrid imeshinda mara 93 ikiwa ni kwenye mashindano yote huku Barcelona imeshinda mara 90

No comments:

Lazaro Masika. Powered by Blogger.