VIDEO: Sky Sports News wameripoti Jose Mourinho kuchukua mikoba ya Lois van Gaal man United msimu ujao.
Bado jina la kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho limekuwa likitajwa kwa ukaribu katika mbio za kuwania nafasi ya kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal, Mourinho amekuwa akiandikwa kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa kama yeye ndio atakuwa mrithi wa Louis van Gaal msimu ujao.
Habari mpya zilizoripotiwa na Sky Sports News leo May 17 2016 ni kuwa kwa zaidi ya mwezi sasa uongozi wa klabu ya Man United umemthibitishia Jose Mourinho kuwa ndio atakuwa kocha wa Man United mwanzo mwa msimu, kama Louis van Gaal akiondoka ndani ya klabu hiyo.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa Mourinho atakuwa na nafasi hiyo kutokana na Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi kutopewa nafasi ya kufanya vizuri akiwa kama kocha wa timu hiyo, kwa muda mrefu sasa Louis van Gaal amekuwa akihusishwa kutaka kufukuzwa na Man United.
No comments: