Baadhi ya wafanyakazi wanaoidai kampuni hiyo wakiwa wamepiga kambi katika Makao Makuu ya ofisi hiyo Jijini Dar Es Salaam.
Erolink ni kampuni inayojishughulisha na tenda ya ajira kwa lugha iliyozoeleka “Out Sources” huku ikisimamia kitengo cha Huduma kwa Mteja “Customer Care Service” ambapo kampuni hiyo ina mambo mengi mabaya yaliyojificha huenda yasipo angaliwa vizuri yataharibu sifa nzuri ya kampuni ya Vadacom.
Kampuni hiyo imechelewesha kuweka michango ya NSSF na PPF pamoja na malimbikizo mishahara katika kipindi cha miaka 2 na miezi kadhaa kwa wafanyakazi ambao waliacha kwa hiyari yao na wengine kuachishwa, mtembezi.com ilifikiwa na kilio cha wahanga hao waliokuwa wakipaza sauti kwamba kampuni hiyo ni ‘jipu’kwani inasifika kwa kutokukusanya kwa wakati michango hiyo hali yakuwa katika “Salary Slip” inaonesha imekatwa.
Madai hayo yameambatana na malimbikizo ambayo Naibu Waziri wa Ajira na Kazi Anthony Mavunde aliwahi kufika kwa ajili ya kutatua tatizo hilo tangu Desemba mwaka jana lakini hadi sasa jitihada hizo zimegonga mwamba baada ya kushindwa kupatiwa ufumbuzi.
Ahadi ya kupata Mafao waliyoitoa Erolink mwezi uliopita kuwa baada ya mwezi mmoja kupita wafanyakazi hao wafike ofisini kwao kuchukua ‘form’ ili zikasainiwe NSSF na PPF ili wahanga hao kupata haki yao imeonekana kuota mbawa walipofika siku ya ahadi na mmoja wa wanaopokea wageni ofisini hapo kuwapa tarehe nyingine ya kupata stahiki zao.
Serikali ya Awamu ya Nne iliagiza wafanyakazi wote wa kampuni ya mawasiliano wapewe kima cha chini cha 400,000, Erolink walikuwa wanalipa chini ya kiwango na unaweza ukapata zaidi ya hapo endapo ukipata ‘Bonus’ lakini kuipata hiyo ‘Bonus’ kazi kubwa sana usiumwe, usipatwe na dharura na ufikie malengo ya simu unazopokea wenyewe wanaita ‘AHT’ madai hayo kuanzia mwaka 2013 hadi 2016, tamko la kulipwa stahiki hizo lilitolewa na serikali Desemba 30, mwaka jana na ilitakiwa utekelezaji uanze Februari Mosi.
Msikilize hapo chini Gelard Sinyangwe Kiongozi wa wafanyakazi wanaoidai kampuni hiyo ya ERO LINK
No comments: