Header Ads


Breaking News
recent

Bondia wa kimataifa  wa ngumi za Kulipwa Francis Cheka maarufu kama SMG  leo amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya shilingi milioni tatu na kumlipa fidia  mlalamikaji mara atakapomaliza kifungo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili kwa kumpiga meneja wake wa baa Bahati Kabanda .
Hukumu hiyo imesomwa na hakimu mwandamizi Morogoro Saidi Msuya baada ya kuridhishwa na ushihidi  uliotolewa na mashahidi wanne katika mahakama hiyo akiwemo mlalamikaji  mwenyewe bw Bahati Kabanda askari polisi ditektivu koplo Richard kutoka kituo kikuu cha Polisi kati mkoani Morogoro mhudumu wa baa ya Vijana Social ya mjini Morogoro aliyokuwa akiimiliki mshitakiwa  Egi Godfrey pamoja na daktari wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro dk Aisha Juma.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Mahakamani hapo hakimu Msuya  ilimtaka mshitakiwa kujitetea na kuiomba mahakama kumwonea huruma lakini kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani ,mahakama ilimwona ana hatia kutokana na kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria  namba mia mbili arobaini na moja kinyume na kanuni ya adhabu na kumhukumu kwenda jela miaka mitatu na mara baada ya kumaliza kifungo kulipa shilingi milioni moja kama fidia na gharama za matibabu kwa mlalamikaji.
Hata hivyo mahakama ilisema mshitakiwa  yuko huru kukata rufaa ndani ya siku thelasini kuanzia leo kwa mujibu wa sheria.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Atuganile Msiyani kuwa mnamo julai mbili mwaka jana  katika baa ya Vijana Social mshitakiwa alimpiga mlalamikaji  Bahati Kabanda ambaye alikuwa meneja wake na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kuzirai na kupelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro kwa matibabu kwa kile alichokuwa akidai kuwa mlalamikaji alikuwa hampatii fedha za mauzo kwenye baa hiyo na kwamba alikuwa akimloga ili asimfuatilie kumpa fedha.
Mwalimu wa kocha huyo Abdallah Komandoo , mdogo wa bondia   Francis Cheka ambaye naye pia ni Bondia Cosmas Cheka na mmoja wa wadau wa ndondi mkoani Morogoro  wanaeleza kuhusiana na hukumu hiyo na nini wanatarajia kufanya huku wakiomba wadau wa michezo ndani na nje ya mkoa wa morogoro kusaidiana katika hilo.

No comments:

Lazaro Masika. Powered by Blogger.