WARIOBA ATOA YA MOYONI "MATUSI NA UONGO BUNGE LA KATIBA VINANIUMIZA"
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wametumia vibaya Bunge hilo kwa kumshambulia na kumsingizia mambo ya uongo kwa makusudi, akisema matusi yanayotolewa dhidi yake yanamuumiza.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja wakati baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na viongozi wa CCM wakiikosoa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba kwa maneno makali,huku wakimshutumu na kumkejeli yeye na baadhi ya wajumbe wa tume aliyoiongoza
No comments: