TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI :
Rais Kikwete achaguliwa Kiongozi Bora Afrika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika
Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013.
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la
kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo itatolewa jioni ya kesho,
Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St.
Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Tuzo
hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango
mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao na limetolewa kwa
Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa
kwa masuala ya utawala bora.
Jarida
hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora chini ya uongozi wa
Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania
kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na
mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.
Jarida
hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji
wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za
jarida hilo.
Linasema
Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji
wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya
kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila
shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake. Na ushahidi
uko kila mahali – ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asili
mia saba kwa miaka yote ya uongozi wake.”
Sherehe
za kesho, miongoni mwa mambo mengine, zitaliwezesha Jarida hilo kutangaza
mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa,
ikiwa ni pamoja na Jumuia ya Kimataifa ya Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi
nyingine zenye ushawishi mkubwa katika medani za kimataifa na zenye makao yake
katika Jiji la Washington na maeneo ya jirani.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
8
Aprili, 2014
No comments: