Header Ads


Breaking News
recent
Matano kuhusu maisha ya Ay




Ay ni miongoni mwa Watanzania ambao wamelibeba sana jina la Bongofleva, akiwa ndio msanii wa kwanza Tanzania kufanya kolabo nyingi na wasanii wa Kenya na Uganda.

Vilevile ni msanii wa kwanza wa Tanzania ambae video zake zimechezwa kwenye kituo kikubwa cha TV cha kimataifa cha Trace TVukiachia MTV Base na Channel O.

Hii ni exclusive kwa DStv.com ambapo Ay ambae amewahi pia kushinda tuzo kwenye Awards za Channel O mwaka 2012, akiwa ni miongoni mwa mastaa ambao hawakuanzia muziki kikawaida Tanzania, amekubali kuongea ya moyoni.



1. Alipotoka nyumbani kwao Morogoro hadi Dar es Salaam kutafuta maisha, hakutaka kukaa nyumbani kwa ndugu kwa sababu alitaka maisha yake na sio kumtegemea mtu.

2. Ay amewahi kulala nje kwa miaka kadhaa Dar es Salaam kwenye stand za Mabasi na pia nje ya kontena ambalo lipo maeneo ya Upanga.

3. Pamoja na kukaa kwake nje, hakuwahi kuwaambia nyumbani kwao kwa wakati huo kwa sababu hakutaka wajue, alijua ni maisha tu yanapita.

4. Kulala kwake nje huku akiwa na begi ambalo alikua anahifadhi vitu vyake mbalimbali kama nguo, kulimfanya awe anakwenda kuoga kwenye mabafu ya jiji ambayo hutoa huduma kwa kulipia.

5. Mama yake mzazi ndio alimpa pesa ya kwanza ya kuingia studio enzi hizo ambayo ni Elfu 20 akitoka Morogoro kuja Dar es Salaam.

No comments:

Lazaro Masika. Powered by Blogger.