FIFA LISTI UBORA DUNIANI: SPAIN BADO 1, TANZANIA YASHUKA 5, IPO 122!!
>>NCHI YA JUU AFRIKA NI IVORY COAST, NI YA 21!!
LISTI YA UBORA DUNIANI YA FIFA iliyotolewa Leo imeonyesha Mabingwa wa Dunia Spain bado wapo Nambari Wani wakifuatiwa na Germany, ambao wamebakia Namba 2, huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 5 na kushika Nafasi ya 122 wakati Nafasi ya Juu kabisa kwa Nchi ya Afrika inakamatwa na Ivory Coast ambao wako Nafasi ya 21wakiwa wamepanda Nafasi 3.
Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka huu, Brazil, wamepanda Nafasi 3 na sasa wapo Namba 6 pamoja na Argentina walioporomoka Nafasi 3.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa tena na FIFA hapo Tarehe 8 Mei.
20 BORA DUNIANI:
1 Spain
2 Germany
3 Portugal [Wamepanda Nafasi 1]
4 Colombia [Wamepanda Nafasi 1]
5 Uruguay [Wamepanda Nafasi 1]
6 Argentina [Wameshuka Nafasi 3]
6 Brazil [Wamepanda Nafasi 3]
8 Switzerland [Wameshuka Nafasi 1]
9 Italy [Wameshuka Nafasi 1]
10 Greece [Wamepanda Nafasi 3]
11 England [Wamepanda Nafasi 1]
12 Belgium [Wameshuka Nafasi 2]
13 USA [Wamepanda Nafasi 1]
14 Chile [Wamepanda Nafasi 1]
15 Netherlands [Wameshuka Nafasi 4]
16 France [Wamepanda Nafasi 1]
17 Ukraine [Wamepanda Nafasi 1]
18 Russia [Wamepanda Nafasi 1]
19 Mexico [Wamepanda Nafasi 1]
20 Croatia [Wameshuka Nafasi 4]
Tanzania bado sana kwenye soka
ReplyDeleteTanzania bado sana kwenye soka
ReplyDelete