EXCLUSIVE:USICHOKIJUA KUHUSU LADY JAYDEE AFUNGUKA KUHUSU GARDNER
Wiki iliyopita tuliishia pale Jide ambaye anaandaa shoo kubwa ya miaka 14 ya muziki wake ya Historia Concert itakayofanyika Mei 2, mwaka huu pale Nyumbani Lounge, Dar, alipokuwa akizungumzia mafanikio aliyoyapata kupitia muziki wa Bongo Fleva. Ishu kubwa ilikuwa ni umiliki wa gari la bei mbaya aina ya Range Rover Evoque. UNGANA NAYE...
Wikienda: Wewe ni mmoja wa wanamuziki waliofanikiwa, je, unaweza kueleza utajiri wako?
Jide: Hapana. Mimi siyo mtu wa matangazo nianze kusema nina nyumba sijui ngapi au magari au nina nini na nini. Cha msingi mashabiki wajue tu Mungu amenisaidia kiasi kwamba nikisema nina kiu, nina uwezo wa kupata maji ya kunywa.

Lady Jaydee akipozi.
Wikienda: Unamiliki gari la bei mbaya aina ya Range Rover evoque, unaweza kutaja bei uliyonunulia?
Jide: Nililipenda tangu lilipotoka nikasema siku moja nitanunua. Kweli nimelinunua lakini siwezi kutaja bei niliyonunulia.
Jide: Nililipenda tangu lilipotoka nikasema siku moja nitanunua. Kweli nimelinunua lakini siwezi kutaja bei niliyonunulia.
Wikienda: Kuna maneno kuwa unawatumia baadhi ya wasanii waliopo upande wako kujiingizia kipato kikubwa zaidi na ndiyo maana wewe una Range Rover wao hawana, hili lipoje?
Jide: Kivipi? Sijafanya shoo zangu na wasanii tangu ile ya miaka 13 ya Lady Jaydee. Kwenye shoo ile kila msanii ambaye alifanya shoo alilipwa. Hakuna aliyefanya shoo ya bure.
Kuhusu kununua Range Rover, pesa nimepata wapi? Jamani nimefanya shoo nyingi mno. Ukiachilia shoo binafsi nilifanya shoo za Kili Tour. Huko sikufanya bure, nililipwa. Kila wiki nafanya shoo na Machozi Band, pesa inaingia, nina mgahawa na miradi mingine.
Wikienda: Nini malengo yako kwa mwaka 2014?
Wikienda: Nini malengo yako kwa mwaka 2014?
Jide: Achana na Ngoma ya Historia ambayo imeshasikika, nimefanya wimbo mpya wa Nitasimama na bado kazi nyingi zinakuja. Mwaka huu nitaendelea kufanya muziki mzuri kwa mashabiki wangu. Pia nitaendelea kuboresha huduma zangu katika shughuli za ujasiriamali.
Wikienda: Idea ya kipindi chako cha Diary of Lady Jaydee kwenye EATV ilikuwa ya nani?
Jide: Gardner ndiye aliyeniambia tunaweza kufanya kitu kama hicho nikakubali kwani niliona ni kitu chema.
Jide: Gardner ndiye aliyeniambia tunaweza kufanya kitu kama hicho nikakubali kwani niliona ni kitu chema.
Wikienda: Kile kipindi kinaonesha maisha yako ya ndani sana. Huoni kama kinakuchoresha?
Jide: Hapana. Siyo mbaya mtu akajua naishije na pale hakuna kitu kibaya. Kwanza sijawahi kufanya vitu ambavyo ni nje ya maadili yetu kisha nikavionesha hadharani. Sipo hivyo.
Jide: Hapana. Siyo mbaya mtu akajua naishije na pale hakuna kitu kibaya. Kwanza sijawahi kufanya vitu ambavyo ni nje ya maadili yetu kisha nikavionesha hadharani. Sipo hivyo.
Wikienda: Umeeleza vitu vingi kuhusu muziki wako, maisha nje ya fani yakoje?
Jide: Naishi kawaida, naona freshi tu kujichanganya na watu wangu, marafiki na mashabiki.
Wikienda: Unaishije na Gardner?
Jide: Naishi kawaida, naona freshi tu kujichanganya na watu wangu, marafiki na mashabiki.
Wikienda: Unaishije na Gardner?
Jide: Gardner ni zaidi ya mume wangu. Tumekuwa wote muda mrefu kiasi cha kujiona kama kaka na dada. Naweza kusema mimi na Gardner ni kaka na dada.
Wikienda: Hujawahi kugombana naye?
Wikienda: Hujawahi kugombana naye?
Jide: Kutofautiana kwenye mapenzi ni jambo la kawaida. Siwezi kusema hatujawahi kutofautiana lakini huwa tunayamaliza wenyewe. Huwa hatupendi mambo yetu yajulikane kwa watu.
Wikienda: Kuna habari ilisambaa siku za nyuma kwamba siku moja ulitoka nduki kwenda kumfumania Gardner maeneo ya Kinondoni-Manyanya, Dar. Je, ni kweli?
Wikienda: Kuna habari ilisambaa siku za nyuma kwamba siku moja ulitoka nduki kwenda kumfumania Gardner maeneo ya Kinondoni-Manyanya, Dar. Je, ni kweli?
Jide: Sijawahi, labda ninyi ndiyo mnanipa umbeya. Ukweli sijawahi kwa sababu tunaaminiana.
Wikienda: Gardner hajawahi kuchepuka mpango wa kando?
Wikienda: Gardner hajawahi kuchepuka mpango wa kando?
Jide: Kwani huko anafuata kitu gani? Mimi naona hakuna jipya huko pembeni. Hajawahi kwa kweli.
Wikienda: Kabla ya kumaliza mfululizo wa makala haya, Jide una jambo lolote ungependa kuwaambia mashabiki wako?
Jide: Waendelee kumsapoti Jide kwani kuna vitu vingi vipya vinakuja. Nawapenda sana!Wikienda: Kabla ya kumaliza mfululizo wa makala haya, Jide una jambo lolote ungependa kuwaambia mashabiki wako?
No comments: