Header Ads


Breaking News
recent

Darassa, Roma Kupiga Shoo Mkesha wa Mwaka Mpya Dar Live

rap-battle

darassa-1

Darassa akisaini mkataba wa mpambano wa Nichane Nikuchane utakaofanyika Mkesha wa Mwaka Mpya (Desemba 31, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live. Kulia ni Meneja wa Dar Live, Juma Mb i z o.
roma-2
Mwana Hip hop R.O.M.A akipitia mkataba wa mpambano wa Nichane Nikuchane kabla ya kuusaini. utakaofanyika Mkesha wa Mwaka Mpya (Desemba 31, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live. Kulia ni Meneja wa Dar Live, Juma Mb i z o.
WAKALI wawili ambao hawashikiki kunako muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ na Shariff Thabeet ‘Darassa’, wamesaini mpambano wa Nichane Nikuchane utakaofanyika kwa mara ya kwanza Mkesha wa Mwaka Mpya (Desemba 31, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live u l i o p o Mbagala-Zakhem jijini Dar.
ILIKUWAJE?
Kwa kipindi kirefu mashabiki wa burudani walikuwa na hamu ya kuwaona wakali hao wakipanda jukwaa moja na kufanya ‘rap battle’ ambapo uongozi mzima wa Dar Live ukaona ni vyema u k a w a t a f u t a wakali hao na kuwasainisha kuingia katika mpambano huo unaokwenda kwa jina la Nichane Nikuchane.
R.O.M.A, DARASSA WATINGA GLOBAL
D a r Live ilifanikiwa kuwapata wakali hao ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita walitinga ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar na kusaini kufanya mpambano huo unaotarajiwa kuwa wa kihistoria.
Akizungumza na tovuti hii, Meneja wa Dar Live, Juma Mb i z o, ali s e m a baada ya k u s a i n i mpambano huo, kilichobaki ni mashabiki kujitokeza kwa wingi Mkesha wa Mwaka Mpya kuburudika na shoo hiyo ambayo haijawahi kufanywa na wakali hao.
“Ni jambo la kumfurahisha kila shabiki wa muziki huu, lengo ni kuwaonyesha mashabiki muziki wa Hip Hop kwa sasa umerudi upya na kujenga heshima. Wale mashabiki wa R.O.M.A anayebamba na Ngoma ya Kaa Tayari na Viva Roma Viva wataburudika naye na hata mashabiki wa Darassa anayetamba na Too Much pamoja na Muziki nao watakata kiu yao.
“Utakuwa ni usiku wa Nichane Nikuchane, weka ngoma hii mi naweka hii ni kama kamchezo ka kuibiana mashabiki na wakati huohuo kuwapa burudani,” alisema Mbizo.
MSIKIE R.O.M.A
Akiizungumzia shoo hiyo, mkali R.O.M.A aliwataka mashabiki wa Hip Hop na muziki wa Bongo Fleva kujitokeza kwa wingi kushuhudia shoo atakayoifanya. “Hii si mara yangu ya kwanza kutimba Dar Live, safari hii nimesaini mpambano wa Nichane Nikuchane na kama mjuavyo sitabiriki na wala sijawahi kumuangusha shabiki yangu yeyote.
Mashabiki watapata kunisikia R.O.M.A wa kipindi hiki cha Magu (Magufuli) nikiwa katika ubora wa kipekee tofauti na vipindi vyote.
“Sipendi kuwa muongeaji sana, ila shoo zangu huwa zinaongea zenyewe. Usikose mwaka mpya kwenye michano nikiwa na debe lililojaa ngoma kama Ivan, Kaa Tayari, 2030, Viva
Roma Viva, KKK na nyingine kibwena,” alisema R.O.M.A.
DARASSA
Naye mkali wa Hip Hop anayetikisa kila kona na Ngoma ya Muziki, Darassa alifungukia siku hiyo kuwa, atawadhihirishia mashabiki wa Hip Hop na Bongo Fleva kwa ujumla kuwa Hip Hop itaendelea kudumu milele.
“Unapozungumzia Muziki wa Hip Hop kwa sasa, unazungumzia ngoma ya Muziki.
Nashukuru ngoma imeeleweka na imepokelewa kila kona ya nchi. Kikubwa nimeshasaini mpambano, hivyo tukutane pale Dar Live nikiikamua kwa mara ya kwanza katika kiwanja hicho.
“Najua mashabiki wamenimiss sana jukwaani hasa Dar Live, hivyo wanangu wote msikose kwani mbali na kuchana ngoma zangu kama Too Much, Heya Haye, Kama Utanipenda na nyingine nyingi, pia nimewaandalia sapraiz kibao,” alisema Darassa.

No comments:

Lazaro Masika. Powered by Blogger.