SHOCKED: UDHAIFU WA BUNGE LA KATIBA, RAIS JK AOMBWA KULIVUNJA HARAKA IWEZEKANAVYO!
BAADA ya kutokea kwa sintofahamu ndani ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kwa wabunge wanaounda umoja wa Ukawa kutoka nje, wengi wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kukivunja chombo hicho.
Tivoli Athuman, mkazi wa Mwenge jijini Dar, alisema ni bora Rais akalivunja bunge hilo kwa vile wajumbe wake wameonyesha udhaifu mkubwa wa kushindwa kutetea hoja zenye masilahi kwa wananchi, badala yake wameweka mbele utashi wao binafsi na vyama vyao.
Mwanamtwa Palango wa Kurasini, alimlaumu Rais Kikwete kwa kuwajumuisha wabunge kwenye bunge hilo maalum, kwani wao ndiyo chanzo cha kukwamisha mambo mengi ya msingi kupata katiba mpya.
“Hakukuwa na sababu ya kuwajumuisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshawaona hawa ni watu wa malumbano tokea mwanzo, kuwaleta huku ni kuvuruga mambo tu, hapa ilibidi Rais ateue mwenyewe wajumbe wasio wanasiasa.
No comments: