NABII: HUYU SI YESU KRISTO WA NAZARETH KAMA WAKRISTO WENGI WANAVYOAMINI BALI HUYU NI.........
Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo amesema picha ya Yesu Kristo inayotumiwa na baadhi ya madhehebu ya Kikrito duniani siyo ya mwokozi huyo wa roho za watu.
Nabii huyo ambaye ana kanisa lake maeneo ya Moshono, Arusha aliyasema hayo hivi karibuni kupitia kituo kimoja cha runinga nchini.
Alisema watu wengi katika ulimwengu huu hawaijui sura halisi ya Yesu Mnazareti bali wamemuona mwigizaji wa sinema za Yesu aitwaye Brian Decon makanisani, majumbani, kwenye biashara, kwenye misalaba na wamemfanya kuwa ndiye mwokozi wao.
“Watu hususan Wakristo wanaiabudu hiyo picha ya huyo mwigizaji anayeitwa Brian aliyeigiza kuwa Yesu. Ni vizuri alivyoigiza, hii imesaidia kufundisha watu kuhusu Yesu kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Injili ya Luka,” alisema Nabii Hebron.
Akaongeza: “Mimi katika maisha yangu pia ufahamu ulitekwa ukaona ile picha ya Brian ndiyo Yesu kutokana na jinsi nilivyofundishwa toka utoto wangu katika madhehebu ya Kikristo.
“Hata sasa inawezekana na wewe unayo picha ya Brian na unaiita picha ya Yesu , hili ni kosa,” alifafanua kuwa cha ajabu ni kuwa ukiingia katika baadhi ya makanisa utaona picha za Brian zimetundikwa ukutani na ndizo watu wanaziabudu.

Alifafanua kuwa, Yesu hakuwa mzee kama huyu muigizaji Brian aliyetumika kuifundisha jamii kwa njia ya sinema ili watu waelewe kirahisi na wapate mfano ilivyokuwa siku hizo. Alijigamba kuwa aliwahi kutokewa na Yesu akaongeza:

Alisema watu wengi badala ya kumuangalia Yesu katika roho sasa fahamu zao zimetekwa na shetani, wanaziona picha za muigizaji kuwa ndiye Yesu na madhara ya kukaa na hizo picha ukutani na kuzibusu ni kwenda kwenye mlango wa kuzimu na kuzisujudia utakuwa tayari umeabudu sanamu,” aliionya dunia.
No comments: